Vidokezo 10 muhimu kwa ufupi ya namna ya kuomba kazi

Maombi ya kazi ni kazi ngumu kuliko wengi wanavyofikiri na hasa kama kazi uombayo ni nyeti na ina waombaji wengi. Zifuatazo ni videkezo muhimu vitakavyoweza kumsaidia mwombaji wa kazi. Ukifuata utakuwa kwenye nafasi muhimu ya kuitwa kwenye usaili na hata kuajiriwa.
  1. Fuata masharti ya kupeleka maombi mfano kichwa cha somo kiweje, utume nini, uambatanishe nini na utume maombi kwa njia gani!
  2. Hata kama hujaambiwa hakikisha hivi vitu viwili ni muhimu, barua ya maombi ya kazi pamoja na CV iliyoandikwa kitaalamu na kwa kufuata weledi wa uandishi wa barua ya maombi ya kazi na uandishi wa CV
  3. Ukituma kwa email hakikisha email ina maelezo yanayojitosheleza ikiwa ni pamoja na kichwa cha somo kinachotaja nafasi unayoomba. Tembelea pia ukurasa huu barua ya maombi kupitia email
  4. Nafasi unayoomba inapozidi kuwa kubwa, ustadi unaoendana na viwango vya kitaaluma ni dhahiri itahitajika katika barua ya maombi pamoja na CV vinginevyo maombi yako yatatupiliwa kapuni
  5. Usimpigie simu mwajiri, kama una maswali ulizia kwa wanamjua mwajiri tarajiwa au tembelea website yao au tembelea ofisi zao kama mgeni wa kawaida sio mwombaji wa kazi ili udodose zaidi kuhusu wao.
  6. Usitume maombi kama wewe huna vigezo vinavyotakiwa kwa maana ya elimu na uzoefu unaotakiwa nk.
  7. Nafasi zenye maombi mengi yana ushindani mkubwa hivyo ili upate hakikisha umefuata maelekezo pamoja na kuandika barua na CV kwa viwango vya kitaalamu zaidi. Kama hujui pata mafunzo husika ya namna bora ya kuandika barua ya kuomba kazi yenye mvuto pamoja na namna bora ya kuandika CV inayokubalika na waajiri wengi. Tembelea pia Namna ya kuandika barua ya maombi ya kazi
  8. Usitume msururu wa vyeti na viambatanisho ambavyo hukuambiwa utume. Hivi mara nyingi utatakiwa kwenda na originals kwenye interview
  9. Usiweke mawasiliano ya ndugu jamaa na marafiki kwenye barua yako ya maombi au CV. Weka ya kwako binafsi na ziwe zinafanya kazi masaa yote. Pia ziwekwe mwanzoni kabisa mwa barua au CV
  10. Usiombe uandikiwe CV au barua ya kazi kwani hiyo itajulikana kwenye usaili na itakuwa aibu na pia hutashinda hiyo interview labda ziwe ni interview za kayumba
 
Vidokeza vitakavyofuata vitajikita kwenye
“Vidokezo Muhimu katika Kuhudhuria Usaili wa kazi”
Hii ni pamoja na maandalizi, kushiriki usaili na mambo muhimu baada ya usaili
Asanteni

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi