Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi kwa KiswahiliJe ulishawahi kuandika barua ya maombi ya kazi na kutuma kwa waajiri wengi na wote au wengi ya hao hawakukujibu hata kama unajua unazo sifa za hiyo kazi?

Jibu la hapo ni rahisi

Uandishi wa barua zako una shida

Barua ya maombi ya kazi iwe na sura hii

  1. Anza kwa kujieleza kuwa wewe nani
  2. Eleza pia umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi, taja gazeti mpaka na ukurasa au kama ni TV/Radio taja ni tangazo la lini ikiwezekana, kama ni website taja ukurasa nk
  3. Eleza kama ukipata fursa ya kuajiriwa unafikiri wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi hawana ila wewe unayo/unazo (Usieleze habari za degree, diploma au vyeti vyako kwani na wenzako wanazo, pia usieleze juu ya uzoefu wako wa kazi kwani na wao wanazo tena kukuzidi). Katika kujieleza kazia zaidi ujuzi wa kipekee na au tabia za kipekee zenye tija kwa taasisi tarajiwa.
  4. Eleza pia utayari wako wa usaili na kuanza kazi
  5. Acha mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba, mama, baba na marafiki au jirani)
  6. Ambatanisha wasifu wako na ueleza kwamba umeambatanisha huo wasifu wako. Angalizo, wasifu usiwe marudio ya barua ya kuomba kazi na barua ya kuomba kazi isiwe marudio ya wasifu wako, vinginevyo haitakuwa na maana