Ujasiriamali ni nini?
Neno ujasiriamali ilianza kutumika miaka ya 1700 likiwa na maana ya kawaida ya kuanzisha biashara.
Lakini wachumi wao wana maana zaidi ya hii.
Kukabiliana na vikwazo za biashara endapo kuna uwezekano wa kupata faida. Kwa wengine ni kuwa na uwezo wa kukwepa vikwazo za biashara ili ufanikishe biashara yenye faida.
Pia wengine wamemuelezea mjasiriamali kama ni mtu mbunifu mwenye uwezo wa kuuza ubunifu wake.
Wachumi wengine wameendelea kumuelezea mjasiamali kama mtu mwenye kuleta bidhaa au huduma za kibunifu kwenye soko ambazo hazijawahi kuwepo.
Katika karne ya 20, mchumi mmoja kwa jina Joseph Schumpeter (1883-1950) alifafanua kuwa mjasiriamali ni mtu mwenye kuleta ubunifu na maboresho yenye kuleta sio tu hamasa bali pia kuwa kichocheo cha mabadiliko.
Joseph Schumpeter aliendelea kumuelezea mjasiriamali kama “mbunifu mharibifu” maana yake ni kwa kuwepo wajasiriamali na bidhaa au huduma zake, viwanda huduma na au bidhaa dhaifu na za zamani zilikufa na kutoweka kabisa kwenye soko.
Mfanyabiashara mtaalamu, Peter Drucker (1909-2005) alielezea wazo hili kwa mapana mengine mapana kuwa, mjasiriamali ni mtu anayepeleleza mabadiliko, kuwa na mwitikio wa haraka na kuhatamia fursa zilizopo katika mabadiliko. Mfano wa hili ni mabadiliko yaliyotokea katika sekta ya mawasiliano kutoka typriter kwenda kompyuta nk.
Wachumi wengi leo hii wanaamini kuwa Mjasiriamali ni moyo na kichocheo katika kukua kwa chumi za nchi mbalimbali duniani.
Mjasiriamali anaweza kutokea katika hali yeyote, msomi au sio msomi, mhandisi, mwanasheria au mwalimu mchungaji au shkhe nk.
Tafsiri ya maneno muhimu
Ugunduzi
Kuleta wazo jpya au bidhaa mpya kabisa kwenye soko
Ubunifu
Kuboresha – Innovation
Ubunifu ni tendo la kuwa na wazo/ndoto/maono na kuyageuza kuwa mradi wa ukweli wa kutatua matatizo ya jamii na kutegemewa na jamii
Ni tendo la kuleta wazo jipya kuwa mradi hai
Kuthibiti mazingira yako – Proactive
Ni kuweza kuyadhibiti mazingira hali zinazokuzunguka pamoja na kuchukua hatua kabla ya uharibifu au madhara kutokea
Kuanzisha biashara.
Tendo la kubuni na kufanya biashara yeyote iliyo rasmi au isiyo rasmi
Kuthubutu – Kukabiliana vikwazo
Kuwa na utayari wa kufanya jambo hata kama kuna vikwazo na hatari nyingi mbeleni zilzo ndani ya uwezo wa mhusika
Uwezo wa kukwepa vikwazo za biashara
Uwezo wa kuchukua mpango mbadala ili kutojiingiza kwenye hatari zilzo nje ya uwezo wako
Kuuza ubunifu
Uwezo wa kuwaambia wengine (wateja) mambo unayoweza kuyafanya ambayo wao wanazihitaji au uwezo wa kuweza kuwaambia wengine (wateja) bidhaa ulizo nazo ambazo wao wanazihitaji
Kuleta bidhaa au huduma za kibunifu /Kuleta ubunifu na maboresho
Kuingiza kwenye soko huduma au bidhaa zenye sio kukidhi hitaji la soko tu bali pia kuhimili ushindani wa soko
Kichocheo cha mabadiliko.
Uwezo wa kuleta vitu vipya kila mara zenye kubadilisha mfumo wa maisha na jinsi watu wanavyoamini, waza, ona na kuishi
Mbunifu mharibifu
Uwezo wa kuleta kwenye soko bidhaa au huduma bora ambazo zina uwezo wa kuviondoa na kuviua huduma na bidhaa hafifu kwenye soko
Anayepeleleza mabadiliko,
Uwezo wa kufanya tafiti na kuyachambua kwa ajili ya kuchukua hatua muafaka na kwa wakati muafaka
Kuhatamia fursa
Uwezo wa kuziona na kuwa wa kwanza kuchukua hatua kwa jambo lolote lenye tija kwako na kwa uma wote
Moyo na kichocheo
Kuwa chanzo cha mabadiliko yeyote yenye tija
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |