Namna Rahisi ya Kupata Mkopo wa Biashara

Namna Rahisi ya Kupata Mkopo wa Biashara

Upatikanaji wa mkopo unategemea sana mahitaji ya biashara yako kimtaji na mtandao wako wa jamaa, ndugu na marafiki na ndugu.

Njia rahisi ya kupata mkopo ni:

  1. Mkopo kutoka kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki  wa karibu
  2. Mkopo kutoka kwenye Taasisi zinazotoa mikopo midogo midogo – MicroCredit Organization
  3. Wakopeshaji binafsi na taasisi zisizorasmi
  4. Mabenki

Mkopo kutoka kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki

Ukifanikiwa katika hatua hii kuna faida lukuki kama ifuatayo

  1. Mara nyingi hazina riba au zina riba ndogo sana
  2. Ukishindwa kurudisha kwa wakati ni rahisi kuongezewa muda wa kurudisha
  3. Mlolongo wa kufuata ili upate mkopo ni mfupi sana

Madhara

  1. Kwa sababu haina masharti magumu ni rahisi mtaji / mkopo kupotea na kushindwa kurudisha kabisa.

Mkopo kutoka kwa taasisi za mikopo midogomidogo – Micro Credit Organization

Hata mikopo inayopatikana kutoka kwenye taasisi kama hizi ni mizuri kwa sababu

  1. Masharti nafuu ya kukopa
  2. Riba ndogo
  3. Haina mlolongo mrefu wa kufuata ili kupata mkopo kama ilivyo kwenye mabenki

Hasara yake

  1. Mkopo unatolewa kwa dhamana ya kikundi na mara nyingi baadhi ya wanachama ni wakorofi hivyo kuna uwezekano wa kumlipia mtu atakayeshindwa kurudisha mkopo na hivyo kikundi kubeba mzigo wa kurudisha
  2. Mikopo inayotolewa ni midogo sana

Wakopeshaji binafsi na taasisi zisizorasmi

Wakopeshaji binafsi ni watu ambao wanatumia akiba ya pesa zao kukopesha kwa riba kubwa ili wapate faida sawasawa na taasisi zisizo rasmi

Wakopeshaji binafsi na taasisi zisizo rasmi zina faida sifuatazo

  1. Haina mlolongo mrefu wa kufuata ili kupata mkopo

Madhara yake

  1. Unaweza poteza mali zako za dhamana kirahisi kama gari, nyumba, ardhi nk
  2. Riba ni kubwa sana kuliko hata benki

Mabenki

Faida yake

  1. Unaweza kopa mkopo mkubwa unaoendana na mahitaji ya biashara yako
  2. Kwa sababu ya masharti magumu na mchakato mrefu, ni ngumu kupata hasara

Hasara

  1. Mchakato ni mrefu
  2. Masharti ni magumu
  3. Riba ni kubwa kwa wengi kuweza kumudu
  4. Unaweza kupoteza mali za dhamana kama nyumba, ardhi nk

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi