Utunzaji wa Vitabu vya Fedha
Utanzaji ni nini?
Kuweka vizuri visiibwe, visiharibike, visiharibiwe, vikitakiwa vipatikane kwa haraka nk
Kama neno linavyosema “vitabu vya fedha” ni moyo wa biashara yako. Vikiibwa au kupotea au kuharibika maisha ghafla hugeuka na kuwa magumu. Fikiria una biashara yako umeisimamia vizuri kwa mwaka mzima au miaka mitatu ghafla vitabu; Vikaibiwa, Vikapotea, Vikanyeeshewa na mvua mpaka vikaharibika vibaya au Vikaungua moto.
Vitabu vya fedha vinatakiwa vikae mbali na uwezekano wa kupatwa na majanga kama ya moto na maji/mafuriko, mvua nk.
Pia viwekwe mbali na uwezekano wa kuibiwa au kupotea, sio kuibiwa tu hata kunakiliwa. Vitabu vya biashara vinabeba siri kubwa ya biashara yako, hivyo viwekwe mahali ambayo ni wahusika wa biashara tu ndio wanajua na kuweza kufikia.
Vitabu vya fedha ni nini?
Vitabu vya fedha ni vitabu wa kutunza taarifa zinazohusu kuingia na kutoka kwa fedha katika biashara yako. Fedha inayoingia ni mapato ya biashara na fedha inayotoka ni matumizi katika biashara yako
Viko vitabu muhimu vingapi ?
Viko vitabu muhimu 7 navyo ni
- Kitabu cha benki
- Kitabu cha stoo
- Kitabu cha mali ya Biashara
- Kitabu cha mapato
- Kitabu cha matumizi
- Kitabu cha mikopo
- Kitabu cha madeni
Jina la kitabu |
Kazi yake |
Umuhimu wake |
Kutunza taarifa za fedha zote zinazoingia na kutoka kwenye account ya benki | 99% | |
Kutunza taarifa za bidhaa zote zinazoingia na kutoka stoo | 50% (sio muhimu kama huna bidhaa za kuweka stoo) | |
Kutunza taarifa za mali zote za biashara kama majumba, magari, fanicha na mashine mbalimbali | 50% (sio muhimu kama huna mali zisizohamishika) | |
Kutunza taarifa za pesa zote zinazoingia kama za mauzo, nk | 100% | |
Kutunza taarifa za pesa zilizotumika katika matumizi ya biashara | 100% | |
Kutunza taarifa za pesa zote unazodai wateja | 99% (sio muhimu kama hukopeshi) | |
Kutunza taarifa za mikopo ulizochukua benki na sehemu zingine | 50% (sio muhimu kama huchukui mikopo) |
Jinsi ya Kuandaa Ripoti ya Fedha
Tembelea ukurasa wa Jinsi ya Kuandika Ripoti ya Fedha hapa
Naomba mkopo wa laki tatu