Business plan
Business plan

Jinsi ya Kuandaa au Kuandika Mpango wa Biashara – Business Plan

Utangulizi

Mpango wa biashara wengine wanauita mchanganuo wa biashara au kwa kimombo “Business Plan” sio kitu kigumu sana kama ukipenda kurahisisha.

Mpango wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biashara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia wawekezaji na watoa mikopo kama mabenki

Mambo muhimu ya kujua katika kuandika Mpangowa Biashara au – Business Plan

Mpango wa biashara wengine wanauita mchanganuo wa biashara sio kitu kigumu sana kama ukipenda kurahisisha.

Ngazi 8 za kufuata ili kutengeneza Mpango wa Biashara

Fuatilia ngazi hizi nane (8), zitakusaidia:

 1. Kasha la nje liwe na kichwa cha taarifa nzima, jina la biashara, muda wa mpango mara nyingi ni kati ya miaka 3 hadi 5
 2. Muhstasari kwenye kurasa moja (Iandikwe mwishoni kwani huu ni maelezo kwa ufupi wa ulichokiandika)
 3. Maelezo ya kampuni au biashara yako, historia ya kuanza, waazilishi, usajili, leseni za biashara, mali nk
 4. Maelezo ya bidhaa au huduma unazotoa au utakazozitoa (Unatenegenezaje, au unaandaaje, usindikaji, ushahidi juu ya udhibiti wa viwango, bei, usambazaji na taarifa ya namna ya kutumia nk)
 5. Maelezo juu ya soko na ushindani (ukubwa wa soko, watoa huduma au wauza bidhaa kama yako, udhaifu na nguvu yao, siri ya wewe/kampuni yako au biashara yako kufanikiwa zaidi yao)
 6. Maelezo juu ya mkakati wa kutekeleza biashara yako (wafanyakazi na mgawanyo wa kazi, Ratiba ya usimamizi, machine, vifaa, mkakati wa kumfikia mteja, orodha ya watoa huduma, nk)
 7. Makisio ya fedha (pesa za kianzio (Startup capital), mtaji (investment) wapi utatoa mtaji?, makisio ya mauzo (Sales forecast),ripoti ya faida na hasara (Profit and loss forecast), makisio ya mzunguko wa fedha katika biashara yako (cashflow forecast), Mchanganuo wa kurudisha gharama na kupata faida (Break even analysis) makisio ya oanisho la mali na madeni ya kampuni/biashara (balance sheet forecast) na Ulinganifu wa sehemu mbalimbali za biashara (business ratios) nk
 8. Viambatanisho muhimu kama Leseni, Cheti cha ulipaji kodi, Cheti cha usajili
  Mikataba, Risiti za mashine, mitambo, ununuzi wa mali za kudumu nk, taarifa mbalimbali za biashara yako ambazo hazikupata nafasi ndani ya mchanganuo huu.  nk

Gharama za kuandaa Mpango wa Biashara

Vigezo vikubwa vinavyoamua ada kiasi gani inahitajika kuandaa mpango wa biashara ni hizi zifuatazo:
 1. Kiasi cha mauzo ya mwaka ambayo unatuhitaji tukuchambulie kwenye BP – BP ya kuchambua Mil 10 ada yake ya kutengeneza ni ndogo tofauti na BP ya kuchambua mil 100
 2. Idadi ya bidhaa/huduma unayotegemea ichambuliwe kwenye BP – Ada ya kuchambua BP ya bidhaa/huduma 1 nio ndogo tofauti na ada itakayotozwa kwenye BP ya bidhaa/huduma 20
 3. Urefu wa miaka ambayo BP itajumuisha kwenye uchambuzi – Ada ya kuchambua BP ya urefu wa miaka 3 ni ndogo tofauti na ada ya BP ya miaka 10 nk

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi