NACTE Certified Curricula

Jinsi ya Kuandika Mtaala au Mitaala ya Vyuo vya Ufundi

Yafuatayo ahpa chini ni hatua muhimu 7 ambazo mtaalamu au mmiliki wa chuo cha ufundi nchini Tanzania atafuata ili kutengeneza mtaala wa kufundishia elimu ya ufundi kwa ngazi kuanzia cheti, diploma na kuendelea.

Hatua na 1

Tayarisha vitu na watu watakaohusika katika mchakato mzima wa kutengeneza mtaala/mitaala husika. Mfano ungehitaji kutumia madodoso, basi andaa hayo madodoso na watu wa kuyasambaza nk.

Hatua na 2

Fanya zoezi la utafiti (Situational Analysis) wa kujua hali halisi ya tatizo unalotaka au chuo tarajiwa inataka kulitatua

Hatua na 3

Tengeneza rasimu ya mtaala au mitaala ambazo utaziwakilisha kwa wadau wa sekta husika ili waboreshe

Hatua na 4

Fanya warsha ya siku moja au mbili itakayowajumuisha wadau mbalimbali wa sekta husika ambao watakuwa na uwezo wa kukosoa, kuongeza, kuondoa na kujadili kwa ujumla rasimu ya mtaala au mitaala uliyoandaa katika hatua na 3 hapo juu

Hatua na 5

Andika ripoti ya warsha na uitume kwa Katibu Mtendaji wa NACTE ikiwa imeambatanishwa na

  1. Barua ya maombi ya kuhakikiwa na kupitishwa kwa mtaala/mitaala husika
  2. Ripoti yenyewe ya warsha (Minutes) pamoja na maoni ya wadau
  3. Rasimu ya mtaala au mitaala iliyoboreshwa na wadau wa warsha
  4. Ripoti ya utafiti (Situational Analysis) uliofanya kwenye hatua na 2

Hatua na 6

NACTE watatuma hati ya madai ya ada ya uhakiki na utatakiwa kufanya malipo haraka na kutuma ushahidi wa malipo kwa Katibu Mtendaji wa NACTE

Hatua na 7

Kuna uwezekano NACTE wakapitia na kugundua mambo kadha wa kadha zinazotakiwa kurekebishwa. Tafadhali uzisome mstari kwa mstari na uzijibu kila swali na jibu lake. Tengeneza pia rasimu ya mtaala au mitaala iliyorekebishwa kufuatia maoni ya NACTE na uzitume ukiambatanisha na barua yenye majibu yote ya NACTE

Baada ya hatua hii ya 7, mtaala au mitaala yako sasa itakuwa tayari, NACTE watakujulisha kwa barua na pia utatakiwa kuchukua cheti cha kupitishwa kwa mtaala au mitaala

Hatua na maboresho

Kila baada ya muda fulani, mitaala inatakiwa kuboreshwa au kuandikwa upya ili kuendana na wakati an mahitaji ya soko, nchi na wadau

Kuna review ndogo na kubwa

  • Maboresho madogo ya mtaala (Minor Review): inatakiwa kufanywa na waalimu muda wowote na NACTE wataarifiwe kuhusu hiyo review ndogo ya mitaala, Curricula Minor Review
  • Maboresho makubwa ya mtaala (Major review): ni maboresho ambayo itaadhiri muundo na mfumo mzima wa mtaala na inatakiwa kufanywa na mtaala pamoja na kuwahusisha wadau wa sekta husika. Aina hii ya review hufanywa kila baada ya miaka mitano (5 years)
  • Kufanya upya mtaala: Mtaala unaweza kuwa umezeeka sana au mamabo mengi katika sekta husika zimebadilika na kwa hiyo huo mtaala utatakiwa kufanywa upya. Kama uhitaji huu ukitokea ni dhahiri hatua zote saba (7) hapo juu ni lazima zifuatwe kama ilivyo.

***Ninafundisha namna ya kuandika kwa urahisi Mtaala wa Vyuo vya Ufundi unaotambuliwa na NACTE kwa vyuo.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi