Bonde la Ngorongoro, Tanzania

Tazama Ramani Utaona Nchi Nzuri, Tanzania

Tazama Ramani Utaona Nchi Nzuri” ni wimbo unaoelezea mali asili na vivutio vizuri vya utalii nchini Tanzania. Nchi yenye mito, maziwa na mabonde mazuri. Ni wimbo pia wa kizalendo kwa wazelendo wa kweli wa Tanzania. Imba wimbo huu kwa moyo wa kweli na rohoni utakuambukiza kuipenda na kujitoa kwa ajili a nchi yako pendwa.

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri

Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,

Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,

Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa

Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,

Kila mara niwe kwako nikiburudika,

Nakupenda sana hata nikakusitiri,

Nitalalamika kukuacha Tanzania.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2  

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,

Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,

Ninakuthamini hadharani na moyoni,

Unilinde nami nikulinde hata kufa.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa

Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

Nyimbo Zingine:

National Anthem of Tanzania | Wimbo wa taifa wa TanzaniaNational Anthem of Tanzania | Wimbo wa taifa wa Tanzania “Mungu ibariki Afrika. God Bless Africa” Performed by Philip Sheppard / London Philharmonic Orchestra. (2012).

Wimbo wa Taifa – Kala Jeremiah fet Nakaaya

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi