Uchimbaji wa Madini Tanzania

Jinsi ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Madini

1.0 Utangulizi

Uchimbaji wa madini ni kuyatoa madini kutoka ndani ya ardhi kuja nje na kuyapa dhamani kwa kukata (vito vya dhamani) au kusafisha (metali) kwa ajili ya matumizi ya binadamu. Uchimbaji wa madini inahusisha pia uchimbuaji wa mawe ya kujengea na dhamani zingine zilizoko ndani ya ardhi. Utaratibu au ustaharabu wa kuchimbua mawe kwa matumizi ya binadamu ulianza pale mwanadamu alipobuni na kuanza kutumia mawe (enzi za ujima) na baadaye metali ya chuma na metali zingine ili kurahisisha kazi . Pia uchimbaji wa madini unajumuisha uchimbuaji wa rasilimali zingine za ardhi kama maji, gesi na mafuta kwa matumizi ya binadamu.

Shughuli za uchimbaji wa madini ndio mojawapo ya shughuli inayoongoza katika kuharibu na kuchafua mazingira na kwa hiyo tathimini ya utunzaji wa mazingira ni muhimu kufanyika kabla ya kuanza kuchimba ili kuweka mpango, mkakati na mbinu za kuhifadhi na kutunza mazingira katika maeneo ya ndani na nje ya mgodi

Kwanza kuna mambo muhimu ni lazima uyafahamu kabla ya kuingia kwenye biashara hii

1.1 Ngazi za Uwekezaji Biashara ya Madini

  1. Makampuni madogo ya uwekezaji, (Uwekezaji wa mtaji chini ya dola za kimarekani milioni 50)
  2. Makampuni ya kati ya uwekezaji (Uwekezaji wa mtaji kati ya dola milioni 50 na milioni 500)
  3. Makampuni makubwa (Uwekezaji wa mtaji wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 500)

a) Makampuni madogo ya uwekezaji – chini ya dola za kimarekani milioni 50

Makampuni madogo ni yale ambazo kwa kiwango kikubwa zinawategemea wenye hisa kununua hisa ndipo zijiendeshe. Nyingi ya makampuni hizi ni za utafutaji wa madini na zinaweza kuwekeza mitaji midogo kwenye uchimbaji mdogo na hivyo kupata mapato yasiyozidi dola milioni 50 kwa mwaka

b) Makampuni ya kati ya uwekezaji dola milioni 50 hadi milioni 500

Makampuni ya kati ni yale yenye mapato kwa mwaka kati ya dola za kimarekani milioni 50 mpaka milioni 500 na hazina uwezo wa kujenga miundo mbinu ya machimbo kama open pit au underground mining sites

c) Makampuni makubwa ya uwekezaji – zaidi ya dola milioni 500

Makampuni yenye mapato ya mwaka ya dola Milioni 500 kwenda juu ndizo zinazohesabiwa kuwa ni makampuni makubwa. Pia ni lazima ziwe na uwezo wa kujenga miundo mbinu ya machimbo kama open pit au underground mining sites bila pesa za nje.

Tuchukulie wewe ni mchimbaji mdogo wa mtaji ulio chini ya milioni 50, sasa unatakiwa pia kujua aina za biashara za madini

1.2 Aina za Biashara za Madini

  1. Utafutaji wa Madini (Mineral Exploration)
  2. Uchimbaji wa Madini (Mining)
  3. Kuchuuza (Brokering or Trading)
  4. Kutoa Huduma na Ushauri (Service and Consultancy)

a) Utafutaji wa madini au Mineral Exploration

Utafutaji wa madini ni biashara nzuri kidogo kwa wale wanaoogopa vihatarishi na pia wanaridhika na faida za wastani. Uwekezaji wake ni mdogo na wa hatua mpaka upate prospect halafu unauza. Hatari yake kubwa iko kwenye kupata mkopo na prospect. Mpaka benki wakupe ni lazima uwe na track record nzuri sio tu ya kuchukua mikopo bali pia ya kuifanya hiyo biashara ya utafutaji kwa asilimia kubwa ya mafanikio.

b) Uchimbaji wa Madini au Mining

Uchimbaji wa madini au mining ni kazi ngumu katika madini kwani kwanza uwekezaji wake ni mkubwa na pia unaweza ukakuta sivyo ndivyo au ndivyo sivyo kule ndani ya ardhi. Vifaa vyako vinaweza kukuonyesha kuna ngema ya kutosha lakini ukizama chini unakuta tofauti. Aidha unakuta ngema kubwa zaidi au unakuta kangema ambacho hata ngarama haiwezikurudisha. Na ndio maana utafiti wa hali ya juu na usio na haraka ni muhimu kabla hujafikia uamuzi wa kuchimba

c) Kuchuuza au trading

Hii ni hatua rahisi kuliko zote kwani hapa unahitaji vitu viwili tu

  1. Utaalamu wa madini unayotaka kuchuuza
  2. Mtaji wa kuanzia

d) Kutoa Huduma na Ushauri (Service and Consultancy)

Hii ni pale unapoamua kutumia ujuzi, uzoefu na vipawa vyako kwa kuwasaidia waliopo au wale wanaotaka kuingia kwenye biashara hiyo.

Huduma zinaweza kuwa ni

  1. Kufanya sorting
  2. Huduma za Umeme na maji
  3. Huduma za usafiri ndani na nje ya mgodi
  4. Huduma za chakula na
  5. Huduma za usafi
  6. Huduma za maduka
  7. Masoko na Kuuza
  8. Kuhudumia vifaa vya uchimbaji
  9. Kuwafundisha wataalamu /wafanyakazi wa migodi nk

2.0 Hatua 9 za Kufuata Ili Kuanzisha Biashara ya Madini

  1. Kusajili Kampuni BRELA
  2. Kijiandikisha Mlipa Kodi
  3. Kuchukua Leseni
  4. Kuchukua Hati ya Usalama wa Mazingira
  5. Kuajiri wafanyakazi na wataalamu wengine
  6. Kununua na kuandaa vifaa mbalimbali
  7. Kutafuta masoko
  8. Kuanza uchimbaji wa majaribio
  9. Kuanza Uchimbaji Wenyewe

1. Kusajili Kampuni

Shirkisha mshauri wa biashara na mwanasheria wa upande wa makampuni ili wakusaidie kwa ushauri na utengenezajiwa MEMART ambayo ni muhimu katika kusajili kampuni

Unaweza kwenda mwenyewe BRELA kusajili au ukamtumia mhsauri mtaalamu wa mambo hayo. Nashauri umtumie mshauri mataalam ili kuokoa gharama za pesa na muda

2. Kijiandikisha Mlipa Kodi kwa kuchukua TIN TRA

Kujiandikisha TIN ni bure na inapatikana kwenye matawi yote ya TRA Tanzania

3. Kuchukua Leseni Wizara ya Nishati na Madini

Baada ya kukamilisha vigezo vya wizara unayo haki sasa ya kuomba leseni ya utafutaji au uchimbaji wa madini ambayo inatolewa na wizara ya Nishati na Madini

4. Kuchukua Hati ya Usalama wa Mazingira

Biashara ya madini ni mojawapo ya biashara inayoharibu mazingira kwa hali ya juu. Ni utaratinu wa mataifa yote duniani kutaka kuwa na uhakika wa utunzaji wa mazingira na hivyo bodi au mamlaka husika watahitaji kuingia mkataba na wewe ili wawe na uhakika kuwa mazingira yatakuwa salama wakati na baada ya uchimbaji.

5. Kuajiri wafanyakazi na wataalamu wengine

Biashara ya madini itahitaji wafanyakazi wa takriban nyanja zote kuanzia wahudumu, maofisa wataalamu na washauri. Hawa wote ni lazima uwaajiri au uwe na uhakika utawapata wapi kwa gharama muafaka

6. Kununua na kuandaa vifaa mbalimbali

Uchimbaji wa madini unatumia technolojia ambazo ndizo zitakazoamua kama wewe ufanikishe mradi au la. Teknolojia ya zamani ianweza kukupa hasara japo rahisi, teknolojia za kienyeji nazo zinaweza kukupa hasara. Teknolojia za kisasa zina faida japo ni ghali kununua. Unashauriwa kuwa na wataalamu washauri wa kukushauri tangu mwanzo namna ya kuamua juu ya teknolojia utakayotumia.

Kwa nini teknolojia za kienyeji au za zamani zina hasara?

  1. Nyingi ya hizo zinatumia muda mrefu kuleta matokeo
  2. Zina gharama kubwa za uendeshaji
  3. Zinaharibu mazingira
  4. Zinahitaji wafanyakazi wengi
  5. Nk

7. Kutafuta masoko

Kulingana na ukubwa wa uchimbaji au utafutaji, ni vyema kutafuta masoko ambayo utauza madini. Ikiwezekana uingie na mikataba ili uwe na uhakika wa kuuza punde utakapovuna.

8. Kuanza uchimbaji wa majaribio

Fanya uchimbaji wa majaribio angalau kwa miezi mitatu hadi sita kwa uchimbaji mkubwa kidogo unaweza kwenda hadi mwaka mmoja. Uchimbaji wa majaribio itakupa fursa ya kujua yafuatayo:

  1. Je vifaa vitafaa kwa malengo yako
  2. Je wafanyakazi uliowaajiri wanaweza kufanya uzalishaji wenye tija
  3. Je biashara nzima italeta tija iliyokusudiwa

9. Kuanza uchimbaji Halisi

Baada ya uchimbaji wa majaribio, sasa unaweza kwa ujasiri kabisa kuanza kuchima madini. Muhimu tu ni kwamba yafanyie kazi changamoto zote zilziojitokeza kwenye uchimbaji wa majaribio

Angalia pia hatua 26 za kuansisha biashara ndogondogo

Save

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi