Vitabu vya Fedha

Vitabu vya Fedha

Utunzaji wa Vitabu vya Fedha

Utanzaji ni nini?

Kuweka vizuri visiibwe, visiharibike, visiharibiwe, vikitakiwa vipatikane kwa haraka nk

Kama neno linavyosema “vitabu vya fedha” ni moyo wa biashara yako. Vikiibwa au kupotea au kuharibika maisha ghafla hugeuka na kuwa magumu. Fikiria una biashara yako umeisimamia vizuri kwa mwaka mzima au miaka mitatu ghafla vitabu; Vikaibiwa, Vikapotea, Vikanyeeshewa na mvua mpaka vikaharibika vibaya au Vikaungua moto.

Vitabu vya fedha vinatakiwa vikae mbali na uwezekano wa kupatwa na majanga kama ya moto na maji/mafuriko, mvua nk.

Pia viwekwe mbali na uwezekano wa kuibiwa au kupotea, sio kuibiwa tu hata kunakiliwa. Vitabu vya biashara vinabeba siri kubwa ya biashara yako, hivyo viwekwe mahali ambayo ni wahusika wa biashara tu ndio wanajua na kuweza kufikia.

Vitabu vya fedha ni nini?

Vitabu vya fedha ni vitabu wa kutunza taarifa zinazohusu kuingia na kutoka kwa fedha katika biashara yako. Fedha inayoingia ni mapato ya biashara na fedha inayotoka ni matumizi katika biashara yako

Viko vitabu muhimu vingapi ?

Viko vitabu muhimu 7 navyo ni

  1. Kitabu cha benki
  2. Kitabu cha stoo
  3. Kitabu cha mali ya Biashara
  4. Kitabu cha mapato
  5. Kitabu cha matumizi
  6. Kitabu cha mikopo
  7. Kitabu cha madeni

Jina la kitabu

Kazi yake

Umuhimu wake

  1. Kitabu cha benki
Kutunza taarifa za fedha zote zinazoingia na kutoka kwenye account ya benki 99%
  1. Kitabu cha stoo
Kutunza taarifa za bidhaa zote zinazoingia na kutoka stoo 50% (sio muhimu kama huna bidhaa za kuweka stoo)
  1. Kitabu cha mali ya Biashara
Kutunza taarifa za mali zote za biashara kama majumba, magari, fanicha na mashine mbalimbali 50% (sio muhimu kama huna mali zisizohamishika)
  1. Kitabu cha mapato
Kutunza taarifa za pesa zote zinazoingia kama za mauzo, nk 100%
  1. Kitabu cha matumizi
Kutunza taarifa za pesa zilizotumika katika matumizi ya biashara 100%
  1. Kitabu cha madeni
Kutunza taarifa za pesa zote unazodai wateja 99% (sio muhimu kama hukopeshi)
  1. Kitabu cha mikopo
Kutunza taarifa za mikopo ulizochukua benki na sehemu zingine 50% (sio muhimu kama huchukui mikopo)

Jinsi ya Kuandaa Ripoti ya Fedha

Tembelea ukurasa wa Jinsi ya Kuandika Ripoti ya Fedha hapa

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi